hii ni dhana potofu na ya hatari hasa ukizingatia baadhi ya wananchi wengi wana mashaka na uzalendo wa watanzania wenye asili ya kiasia 
 anatumia vita dhidi ya ufisadi kupanda mbegu ya ubaguzi alisema profesa lipumba 
 alisisitiza maamuzi na kutowajibika ndani ya serikali ndiyo chanzo cha kuongezeka kwa rushwa na siyo wahindi wachache 
 tukipanda mbegu za ubaguzi wa rangi tutateleza na kuingia katika ubaguzi wa kidini na wa ukabila alisema profesa lipumba 
 akizungumzia utendaji kazi wa serikali ya rais kikwete alisema imeshindwa kuwatumikia watanzania kutokana na kukosekana uongozi madhubuti na utawala bora